MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia huru mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 au kwenda jela miaka miwili kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya, ambapo amefanikiwaa kulipa pesa hizo na kuachiwa huru.
Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.