expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Thursday, August 21, 2014

Kuhusu Mtoto Wa Jackie Chan Kukamatwa Na Marijuana

chanMtoto wa star wa filamu mkubwa duniani Jackie Chan ‘Jaycee Chan’ ambaye pia ni muigizaji ameripotiwa kukamatwa na gramu 100 za marijuana kwenye nyumba yake. Kitendo hichi kimekuja kama mshtuko mkubwa kwa baba yake ambaye aliwahi kuwa balozi wa kampeni ya kupinga uuzaji,usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana mwaka 2009.
Jackie amesema “hii ni aibu kubwa kwake kama mtu wa watu na baba mzazi, Jaycee
amenivunja moyo sana, nimeshindwa kumwelimisha mwanangu na kwa niaba ya jina la mwanangu naomba kumwombea msamaha kwa uma” alisema Jackie Chan.

No comments:

Post a Comment