Thursday, February 27, 2014
Wednesday, February 26, 2014
Diamond kwa wasanii wanaomchafua: Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba, mie sijui, sina tatizo, ila niacheni
Diamond Platnumz ameamua kufunguka ya moyoni kuhusiana na kile alichokieleza kama kusemwa vibaya na wasanii wenzake ilihali yeye amekuwa akifanya mambo kimpango wake.
“Kiukweli, nasikitishwa sana jins baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media, Mara sjui Nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu….kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika… mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu…” Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui “sinatatizo… Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya “Sina tatizo”… sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu… Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu….. Watu wanataka kazi,” ameandika kwenye Instagram.
Tuesday, February 25, 2014
Hii stori ya maisha ya mwigizaji Masanja inaweza kukutoa machozi. Amkumbuka Marehemu Kanumba
Masanja Mkandamizaji si jina geni masikioni mwa watu wengi kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu watazamaji pale anapoonekana katika runinga na Kundi la Original Comedy. Licha ya kufika hapo alipo sasa, anakiri wazi kuwa amepitia katika maisha magumu hususani wakati alipoamua kuanza maisha binafsi ya kujitegemea baada ya kutoka nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi.
Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake alimuomba amtafutie chumba ili ajitegemea na kuanza maisha binafsi kama kijana . Nilimwambia dada anitafutie chumba na alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya Tabata Aroma na nilitakiwa kulipa kodi ya TSh. 5,000 kwa mwezi, anasema Masanja. Anakiri wazi kuwa changamoto katika maisha ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa kwani licha ya kuwa katika hali ngumu Hakukata tamaa bali alizidi kujituma kwa nguvu zake zote. Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata hata hiyo hela ya kodi kwahiyo ilikuwa inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda unapofikia wakati kulipa kodi. Yaani hiyo TSh. 5,000 kuipata ilikuwa shughuli maana ilikuwa ikifika karibu na mwisho wa mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo ili mama mwenye nyumba ajue nimesafiri,anasema. Anasema alianza kwa kulala chini mpaka siku alipofanikiwa kupata fedha kidogo iliyomuwezesha kununua godoro la sufi jambo ambalo anajivunia nalo kwani aliweza kununua kwa jasho lake. Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau marehemu Steven Kanumba pamoja na mtu mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na mchango wao uliosaidizi kumfikisha hapo alipo sasa. “Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa anakuja kunichukua kule Tabata tunaenda kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia pesa kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha yalikuwa magumu. Wakati naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata ya kununua chipsi kavu lakini siku moja nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki moja sikuamini macho yangu, kwa mara ya kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa nikitamani mlo huo nililazimika kusaidia kumenya viazi kwa washikaji” alieleza Masanja. Sambamba na uchekeshaji Masanja pia amejiingiza katika shughuli za kumtukuza Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya vizuri pia katika uimbaji wa nyimbo za injili na kesho Jumapili atazindua albamu yake ya pili ya muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini ya jua.
-Habari kwa hisani ya mwandishi John Minja-