
HAWA NDIYO WALISHAMBULIWA KWA BOMU NA KUOFIWA KUFA
BAADHI YA MAJERUHI WA BOMU LAKUTUPWA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA SOWETO
HIZI NI DAMU ZILIZOTAPAKA HAPA CHINI
HIZI NI DAMU ZILIZOTAPAKA HAPA CHINI
HIZI NI DAMU ZILIZOTAPAKA HAPA CHINI
BAADA YA BOMU KAMANDA MBOWE AKIFANYA JUHUDI ZA KUWATAFUTIA USAFIRI MAJERUHI
WANANCHI WAKIWA WAMEPIGWA NA MSHANGAO BAADA YA BOMU KULIPUKA
BAADA YA BOMU KAMANDA MBOWE AKIFANYA JUHUDI ZA KUWATAFUTIA USAFIRI MAJERUHI
BAADA YA BOMU KAMANDA MBOWE AKIFANYA JUHUDI ZA KUWATAFUTIA USAFIRI MAJERUHI
LEMA AKIWA NA MBOWE WANAJADILIANA BAADA YA BOMU KULIPULIWA
MWESHIMIWA MBOWE AKIKIMBIA BAADA YA POLISI KUANZA KUPIGA MABOMU YA MACHOZI
PICHANI NI BOMU LA MACHOZI LILILORUSHWA NA POLISI BAADA YA TUKIO LA BOMU
AWALI KABLA YA TUKIO HILO MAKAMANDA WAKIWA JUKWAANI
LEMA AKIONGE NA WANANCHI
WATU WAKIWA WAMEACHA NJIA HILI KAMANDA APITE
KAMANDA MBOWE AKIWA ANAINGIA
Uwanja wa
Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata
ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa
vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na
zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.
Katika
Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema naa Mbunge wa Arusha
Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa
Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa vinara katika
Mkutano huo hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.
Mlipuko
huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara
baada tu ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka
chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu,
hali inayoashiria mrushaji huenda lilenga kuwajeruhi viongozi hao.
Miili ya
marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini
hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya
wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuwawa.
Baadhi ya
majeruhi ni viongozi wa Chadema ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa wa Arusha,
sambamba na wananchi wa kawaida wakiwemo watoto waliofika mkutanoni
hapo.
Mkutano wa
leo ulivunja rekodi ya mahudhurio viwanjani hapo.. lakini ulikuja
kuharibika baada ya kutokea mlipuko huo haotuba zikiwa zimeishamalizika
na baadhi ya watu wakiwa wanatawanyika kuelekea majumbani huku zoezi la
kuchangisha pesa likiendelea, kitendo kilichowazuia hata wakusanyaji
michango kushindwa kumalizia zoezi hilo…
Hali ikiwa
bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku
askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi
kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa
na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.
Kijana
mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo
alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na badae kukimbilia nyumba
zilizojirani.
Mwenyekiti
wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya
Kaloleni Jijini Arusha jioni ya leo katika Mkutano wa Chadema kufunga
kampeni zake.
Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea
No comments:
Post a Comment