WATU wawili ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , waliofariki jana baada ya kulipukiwa na bomu katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Udiwani kata ya Kaloleni,jijini Arusha, mmoja ametambuliwa na mwingine bado hajafahamika.
Mganga,
mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Arusha, Dakta Josiah Mlay, amemtaja
marehemu huyo kuwa ni Judith Mushi, (46) mkazi wa Sokon one jijini
Arusha, na mwingine ni kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa
miaka kati ya 15-16 ambae hajafahamika ambae alifia hospital ya AICC.
Dakta
Mlay, amesema katika tukio hilo hospital hiyo imepokea majeruhi 10 kati
ya 15 na wote ni wanaume isipokuwa majweruhi mmoja wa kike aitwae
Sharifa Jumainne ,ambae hali yake ni mbaya.
Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali imegundulika kuna kuipande cha chuma kwenye mapafu ambacho kinatokana na mlipuko wa bomu
Aidha
amesema kuwa majeruhi mwingine aliyepata majeraha ya kichwa
amehamishiwa kwenye hospital ya Seliani ya Arusha kwa uchunguzi zaidi
akisubiriwa kupelekwa hospital ya rufani ya KCMC ya mjini Moshi.
Dakta Mlay, amesema hali za majeruhi wengine waliolazwa hospital ya mkoa wa Arusha ya mount Meru, zinaendelea vizuri.
Wakati
huo huo tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Arusha, imeahirisha uchaguzi
huo hadi June 30 mwaka huu kutokana na tukio hilo la mripuko wa bomu
lililojeruhi watu .
Katika
hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amewatembelea
majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospital mbalimbali za mkoani
Arusha zikiwemo mount Meru, Seliani, na AICC .
Katika
hatua ingine viongozi mbalimbali w a chadema wametembelea katika eneo
la tukio akiwemo mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema
Freeman Mbowe na wabunge wa jimbo la Arumeru pamoja na Arusha mjini.
No comments:
Post a Comment