MWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe
amesema tukio la mlipuko wa bomu lililoua watu wawili juzi mkoani
Arusha, lilimlenga yeye na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mbowe
alisema bomu hilo ambalo liliambatana na milio ya risasi lilikusudiwa
wazi kuondoa uhai wake, jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa taifa.
Alisema
katika tukio hilo, kulikuwa silaha za aina tatu ambazo zilitumika,
ukiondoa bomu, kulikuwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) na
bastola.
“Waliopanga unyama ule walilenga kutuua sisi, waliokufa wamekufa kwa niaba yetu,
“Watu
hawa, waliandaliwa na wengine walikuwa katikati ya umati wa watu,
waliokuwa pembezoni mwa uwanja, tumebaini wanalindwa na polisi,
“Risasi
za SMG zilitoboa tanki la mafuta la gari letu la matangazo, ambalo sisi
tulikuwemo juu, lengo likiwa baada ya bomu kulipuliwa,tanki nalo
lingelipuka,
“Hawa walitaka kufanya mauaji halaiki, ikiwemo sisi viongozi wa Chadema, Mungu bado anatusimamia,”alisema
Alisema majeruhi wote ambao wamelazwa, bado wana vyuma vingi milini mwao kutokana na kujeruhiwa vibaya.
“Tumepiga
picha makasha ya risasi na kuyakabidhi polisi,bado tunaamini,kwa sababu
tukio hili halihitaji mashine ya kiuchunguzi ya mwezini vyombo vya
usalama, vitatoa taarifa mapema,”alisema Mbowe.
Kutokana na msiba
huo, Mbowe alitangaza kuwa wabunge wa chama hicho, wote kuanzia leo
hawatashiriki mkutano wa Bunge la Bajeti hadi marehemu watakapozikwa.
“Msiba
huu, umekigusa chama,wanachama,wapenzi na wananchi wote wa
Tanzania,wabunge wote watakuwa bega kwa bega na wananchi wa Arusha mpaka
watakapopumzishwa marehemu,”alisema Mbowe
Alisema mazishi ya
marehemu wote, yatafanyika kitaifa kwenye Viwanja vya Soweto, kabla ya
marehemu wote kusafirishwa na ndugu zao.
“Chama kinauchukulia
msiba huu kama msiba wa taifa,tumeamua kupiga mahema katika uwanja ule
na marehemu wataagiwa hapo ambapo moja ni atazikwa Kilimanjaro na
mwingine Tabora”
“Tukio hili ni la kisiasa na limepangwa,
ninawataka wenzetu kama shughuli za siasa zimewashinda wafute mfumo wa
vyama vingi ili wananchi wasio na hatia wasiendelee kufa”
Alisema chama kitafanya harambee kuchangia majeruhi kwa ajili ya matibabu yao.
No comments:
Post a Comment