Mtuhumiwa Bomu Kanisani, Asomewa mashtaka 21
Mtuhumiwa Bomu Kanisani Arusha, Victor Ambrose Calist (20).Joseph Pantaleo, Arusha Tanzania
Arusha kumekucha, mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka 21 ya mauaji na kujaribu kuua.
Kesi ya mshtakiwa Victor Ambrose Calist (20) ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo jijini Arushai amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu mkazi, Devotha Kamuzora.
No comments:
Post a Comment