amebaki masaa kiduchu kabla Afrika haijawaona Live washiriki wa Big Brother Africa 2013 ambayo imepewa jinaThe Chase. Lakini wakati kila mtu akisubiri kwa shauku kujua ni kina nani watakuwa ndani ya Jumba kuwania donge nono la Dola Laki Tatu ($300,000), hizi hapa ni picha ambazo zinakuonjesha japo kidoogo jinsi ambavyo jumba la Big Brother Africa lilivyo.
Inaaminika kwamba jumba lina camera 56 na vinasa sauti 137 kitu ambacho kinamuwezesha Biggie kuwaona washiriki 24/7.
Big Brother Africa 2013 inaletwa kwa udhamini wa Airtel na kuandaliwa na Endemol. Shindano litakuwa linaonekana masaa 24 kupitia DStv kwenye channels 197 na 198.
No comments:
Post a Comment