“Wizara yangu kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara tutafanya uchunguzi, tukijiridhisha tutapiga marufuku pombe hiyo,” alisema. Dk. Mwinyi alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu, Lediana Mng’ong’o (CCM) aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kupiga marufuku pombe hiyo. Mng’ong’o alisema pombe hiyo imekuwa na athari kubwa katika jamii hususan kundi la vijana ambao baadhi wamekuwa wakishinda vijiweni bila kujitambua. Mbunge huyo alisema si tu pombe hiyo inaathiri afya za watumiaji, lakini pia imekuwa ikiathiri shughuli za uzalishaji mali katika jamii. Akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake, Dk. Mwinyi alisema anatambua madhara kutokana na matumizi ya pombe ya viroba. “Tutalifanyia kazi suala hilo, tunatambua kuwa pombe ina madhara makubwa kwa afya na jamii. Kijamii pombe imekuwa moja ya vyanzo vya ajali barabarani,” alisema. Source: Gazeti la Tanzania Daima May 11,2013, mwandishi ni Khamis Mkotya, Dodoma
Saturday, May 11, 2013
GAZETI LA MTANZANIA:POMBE YA KIROBA KUPIGWA MARUFUKU

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment