expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Sunday, April 21, 2013

Dawa za kuongeza akili zaingia nchini


Mtindo wa maisha, ulaji na msongo wa mawazo, vimewasababishia Watanzani wengi maradhi lukuki hata vifo.
Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu, kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana kijana.

Wabunge wa Chadema kuweka kambi majimbo ya Makinda, Ndugai


Mwanza. Wabunge sita wa Chadema waliosimamishwa bungeni wameamua kwenda kuwashtaki Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai kwenye majimbo yao.

HOJA: KAMA WABUNGE WANAONGEA MATUSI BUNGENI, KWANINI WANAFUNZI WASICHORE MAZOMBI KWENYE MITIHANI YAO.



Bunge letu linaelekea wapi jamani, Yaani wabunge waliopewa idhini na wananchi wao ili kutetea maslahi ya wananchi wao hivi sasa ndo wamekuwa viongozi wa kutukana matusi bungeni. Vitendo hivi vya kusikitisha vinaonyesha dhahiri kuwa kwa sasa Elimu ya Uzalendo hapa Nchini kwetu inaelekea kupotea, Wimbo wa chuki na Udini umeonekana kutawala midomoni mwa Wengi hivi sasa.

Friday, April 19, 2013

MAKINDA KUAMUA HATIMA YA LISSU LEO


Chanzo cha kutimuliwa ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba (CCM).

Wednesday, April 17, 2013

HI KATUNI NILIIKUTA KWENYE MWANANCHI.CO.TZ


Bungeni kwachafuka tena,Lema achafua hali ya hewa bungeni


Dodoma.Wabunge watano wa Chadema jana walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano kutokana na vurugu zilizotokea jana usiku.

BREAKING NEWS:BI KUDUDE AFARIKI DUNIA



Mwanamuziki maarufu na mwenye umri mkubwa kuliko nchini Tanzania, Bi Kidude, amefariki dunia leo hii akiwa Zanzibar, alikuwa anaumwa na alipowahishwa hospitali haikuwa rizki tena.
 Taarifa ya kifo chake ilitolewa na mpwa wake Baraka Abdulrahman Alisema Bi Kidude alifariki hospitalini kutokana na maradhi ya kisukari na uvimbe kwenye Kongosho.

Bi Kidude amekuwa katika fani ya muziki wa taarab ya kiasili pamoja na ngoma za unyago kwa zaidi ya robo tatu ya umri wake.
Katika miaka ya karibuni afya yake imekuwa ikizorota kiasi cha serikali ya Zanzibar kumzuia kupanda majukwaani kuburudisha japokuwa alionekana katika tamasha la Sauti za Busara mwezi Februari mwaka huu.
Mipango ya mazishi ya nguli huyu inafanywa nyumbani kwake Zanzibar

mambo kumi muhimu ya kufahamu,na utafiti umefanyika




1. Huko Hong Kong mwanamke anayemfumania mumewe akifanya mapenzi na mwanamke mwingine anaruhusiwa kisheria kumuua mwanaume huyo lakini kwa mikono yake pasipo kutumia silaha yoyote.
2. Watu toka Ugiriki wana wastani wa kufanya mapenzi mara nyingi kuliko watu wote duniani wakiwa na wastani wakufanya tendo hilo mara 145 kwa mwaka huku Wajapan wakiwa na wastani mdogo wa kufanya mapenzi mara 45 kwa mwaka.
3. Kujilazimisha kusahau kitu au kumsahau mtu fulani kunakufanya uwaze kuhusu kitu hicho au mtu huyo mara 100 zaidi.
4. Mashairi ya nyimbo za muziki huwa na mchango mkubwa kwenye ubongo wa mtu mwenye huzuni .

5. Mwanamke mmoja huko Uingereza mwaka 2005 alijifungua mapacha ambao walikuwa wanatokana na wanaume wawili tofauti yaani kilanpacha na baba yake,hii hutokea mara mojakwenye kila kesi 13,000.
6. Maumivu ya kihisia ambayo humpata mtu pindi anapoachana na mpenzi wake yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo.
7. Maumivu anayopata mwanamke wakati wa kujifungua yamethibitishwa kuwa sawa na maumivu ya mtu anayeungua moto huku akinishuhudia.
8. Tajiri wa Marekani Bill Gates hutumia zaidi ya dola laki saba na elfu arobaini kila mwezi  kugharimikia nyumba yake ya kifahari.
9.Utafiti umeonyesha kuwa wakati mtu anapolia kwa uchungu chozi la kwanza hutoka kwenye jicho la kushoto,kinyume chake ni kwamba kila pale mtu anapolia kwa furaha chozi la kwanza hutokea jicho la kulia.
10.Utafiti uliofanywa kwa mashabiki wa mwanamuziki Justin Bieber umeonyesha kuwa mashabiki wanne kati ya watano ambayo ni sawa na asilimia zaidi ya 90 wanakumbuka majina ya nyimbo zake zote na hata mashairi lakini hawakumbuki jna la mji mkuu wa Iraq
source:millardayo.com


MSANII JB KUGOMBEA UBUNGE

Msanii namba 1 wa bongo movies Steven Jacob(JB) mwanye heshima kubwa sana hapa nchini na nje ya nchi kwa kazi zake nzuri anazozifanya,amesema yuko mguu sawa kugombea UBUNGE mwaka 2015.
amesema hiyo ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingi.ila hajatamka hasa ni jimbo gani atakalo gombea ila atatamka baadae.

angalia,MHINDI kavaa shati la dhahabu tupu lenye uzito wa kilo 3.na lina bei kuliko yote duniani.Gharama yake ni sawa na shilingi milioni 450 za kitanzania


story za kwenye facebook





Tuesday, April 16, 2013

hawa vijana wanjiita FIRM

                                                       (Edu,Samweli n George)

hawa vijana wanajiita FIRM,kama ulikuwa hujui inasemekana kuwa ni wataalamu wa ECONOMICS na ACCOUNTS.kama unashida ya accounts au uchumi Advanced level watafute.

PICHA MBILI ZA GARI JIPYA LA 50 CENT

     

Monday, April 15, 2013

Bungeni hakukaliki,kauli za kejeli na za kuudhi zatawala



Dodoma.Baadhi ya wabunge jana waliendelea kutumia fursa ya mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu kurushiana vijembe na maneno ya kuudhi mambo ambayo yalisababisha mivutano ya kikanuni, huku mmoja wao akionya kwamba ikiwa haki hiyo itaendelea bungeni hakutakalika.

Chimbuko la mivutano hiyo ni kauli zilizotolewa na Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM), Juma Nkamia ambaye alimjibu Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi kwamba “haongei na mbwa bali anazungumza na mwenye mbwa.”

Kadhalika Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde aliwapiga vijembe viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akisema kwamba kuna wabunge ambao wana “mimba zisizotarajiwa bungeni”.

Vijembe hivyo viliendelea jioni baada ya Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje kusema Serikali iliyopo madarakani haina uwezo, haina ujuzi na imepoteza imani ya watu kutokana na kushindwa kuwatatulia wananchi matatizo yaliyopo.
Naye Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa akieleza kuwa Serikali ina tatizo kwa kuwa kuna “akili ndogo inatawala vichwa vikubwa.”

Alitumia kifungu cha kitabu kitakatifu cha Biblia cha Mithali 27:22 kinachosema kuwa “mpumbavu ukimchukua ukimchanganya na ngano kwenye kinu atabaki na upumbavu wake.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Wenje na Msigwa walikiuka kanuni za Bunge kutokana na matamshi yao.

Naibu Spika, Ndugai alionya lugha hizo bungeni akiwasihi wabunge kuacha kutumia, kauli iliyoungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Anna Abdallah ambaye alieleza kukerwa na udhalilishaji wa wanawake bungeni.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Paulina Gekul akitumia Kanuni ya 68 (7) alikilaumu kiti cha Spika kwa kukaa kimya wakati wabunge wanatukana bungeni. “Kama hali hii itaendelea, humu ndani kutakuwa hakutawaliki,” alisema Gekul.

Pia Moses Machali (Kasulu Mjini -NCCR-Mageuzi) na Magdalena Sakaya (Viti Maalumu-CUF) waliomba mwongozo wa Spika wakitumia Kanuni ya 64 inayozuia lugha za kuudhi bungeni.
Lusinde alianza kuipiga vijembe hotuba ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na baadaye alidai kwamba wapo wabunge wenye mimba zisizotarajiwa ambao wanaharibu nchi.

“Ukiangalia kuna watu wanataka kuvuruga nchi wakati wana watoto wachanga. Mimi mtoto wangu wa mwisho ana miaka minane halafu Slaa (Dk Willibrod, Katibu Mkuu Chadema) wa kwake sijui ana wiki ngapi,” alisema Lusinde na kuongeza: “Hawa wapinzani tuachieni mimi na Mwigulu (Nchemba, Naibu Katibu Mkuu CCM).”

Baada ya Lusinde kumaliza Sakaya aliomba mwongozo wa Spika kuhusu utaratibu akitumia Kanuni ya 64(1) (g) , akisema kauli yake kwamba kuna wabunge ambao ni viongozi wana mimba zisizotarajiwa ni ya kuudhi.