expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>

Tuesday, September 24, 2013

Hii ndio video ya Criss (Mzungu) akiimba wimbo wa Diamond "Mbagala", na kuutafsiri kwa kizungu



Hiki ndicho alichokiandika Criss juu ya kuimba wimbo huu

As a language exercise, I picked a Swahili pop song that I like and attempted to transcribe the lyrics and learn to sing it. The Swahili lyrics are below as well as my attempted English translation. Mbagala is an impoverished district on the outskirts of the Tanzanian city Dar Es Salaam. I might have made some mistakes in the transcription or translation, so kama wewe ni Mswahili na unalo shauri lolote kuhusu maneno au tafsiri, niambie!

OMY DIMPOZ..!!POOZZ KWA POOZZZ NDANI YA VOICE OF AMERICA

Ommy Dimpoz ambae  yuko Marekani kwa ajili ya shows kadhaa ndani ya wiki 3 zilizompeleka huko, amepata nafasi ya kuhojiwa na kituo cha VOA, na kuzungumza mengi juu ya muziki wake.

Dimpoz akihojiwa na mtangazaji wa kituo hicho "Sunday Shomari" ambapo alizungumzia kuhusu matatizo ya wasanii kutumia madawa ya kulevya nchini, historia yake katika kazi yake ya muziki, tour iliyompeleka huko, malengo yake ya baadae na mengine mengi.
Dimpoz anatarajia kuanza show yake ya kwanza ndani ya Washington DC siku ya kesho na tayari mpaka sasa meza za VIP zimeshauzwa zote na kiingilio chake ni dola 30 kwa wale wa kawaida

Tuesday, September 3, 2013

DAYNA -BEAT YA ‘MY NUMBER ONE’ YA DIAMOND PLATNUMZ NI YANGU.

Nyota wakike wa muziki wa kizazi kipya anayefahamika kwa jina Dayna Nyange ameibuka na malalamiko zidi ya mwanamuziki Naseeb aka Diamond Platnumz.
Baada ya Dayna kuomba collabo kwa Diamond Platnumz na kukubaliwa na msanii huyo kutoka Wasafi Entertainment, kwa kigezo cha kumuachia wimbo Diamond ili aweze kuufanyia mazoezi.

Kwa sasa imekuwa ndivyo sivyo kwa Wasanii hao kuibiana kazi baada ya tetesi hizo mwandishi wa Baabkubwa ikamvutia waya Dyana Nyange ili kujua ukweli wa tetesi hizo”Mimi mashairi si yangu bali beat ndiyo yangu na wimbo niliutengenezea studio ya Burn Record chini ya producer ShedCrever, baada ya kukamilika nilishauriana na producer mtu wa kushirikiana nae ndiyo akaniambia nifanye na Diamond Platnumz, so nikamtafuta Platnumz akaniambia niende kwake ndipo nikaamuamua kumuachia wimbo wangu baada ya kukutana nae”.
Baada ya hapo alitafutwa producer Shade crever na Diamond hawakupatikanika kwenye simu zao.  
source;Baabkubwa magazine

official video>diamond platnumz;my nomber one