kushoto ni Batuli na kulia ni Irene Uwoya
Hii ni picha ya hivi karibuni ambayo imetoka ikiwaonyesha waigizaji maarufu wa Swahili movies Yobnesh Yusuph(Batuli) na Irene Uwoya. Hapo ilikuwa katika set ya filamu mpya inayokuja inaitwa Bad Luck Batuli akiwa mmoja wa waigizaji wakuu, Uwoya hayupo kwenye hiyo filamu ila alipita tu kuangalia wenzake wanafanya nini. Hawa waigizaji wote wawili ni maarufu, wazuri na warembo, pia wote wameigiza kwenye filamu nyingi na mastaa mbalimbali, kwa mara ya kwanza Irene Uwoya alijipatia umaarufu baada ya kuigiza katika filamu ya Oprah akiwa na Ray na marehemu Kanumba wakati Batuli alijipatia Umaarufu baada ya kuigiza filamu ya Fake Smile akiwa na marehemu Steven Kanumba. Batuli ni mama wa watoto wawili mmoja ana miaka 9 na mwingine miaka 5 wakati Irene Uwoya ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 2. Ukiachana na hayo yote nani unahisi ni mkali katika urembo, suala zima la fashions na kuigiza kwa ujumla bila kujali umaarufu wao au wingi wa filamu walizoigiza?
No comments:
Post a Comment