Diamond Platnumz akiwapa hi mashabiki.
Nyomi iliyoitikia shoo hiyo.
Diamond na Ney wakiwapagawisha mashabiki.
Ney wa Mitego akisema na wapenzi wake.
Diamond Platnumz akionyesha umahiri wake stejini.
Diamond akifanya makamuzi sambamba na kundi lake.
Diamond na kundi lake katika pozi kabla ya makamuzi.
–
DAR Live usiku wa kuamkia leo ilitikisika baada ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho la pamoja kati ya wanamuziki wawili nyota wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ney wa Mitego ambao walikuwa wakizindua video ya wimbo wao wa ‘Muziki Gani’.
Wanamuziki hao kwa pamoja walitoa burudani ya nguvu ambayo ilizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika katika ukumbi huo wa maraha uliopo Mbagala Zakhem, jijini Dar.
No comments:
Post a Comment